Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuweka Muda kwa Ajili ya Marafiki katika Familia

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuweka Muda kwa Ajili ya Marafiki katika Familia

  1. Kuweka muda maalum kwa ajili ya marafiki katika familia: Ni muhimu kwa familia kuweka m... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kujisahau katika Mahusiano: Kuweka Thamani ya Kujipenda na Kujali

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kujisahau katika Mahusiano: Kuweka Thamani ya Kujipenda na Kujali

Mahusiano ni jambo la kawaida sana kwa kila mtu. Tunapenda kujenga uhusiano na watu ambao tunaowa... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha uhusiano na marafiki

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha uhusiano na marafiki

  1. Kuwa Mchangamfu Katika kujenga na kudumisha uhusiano na marafiki, ni muhimu kuwa mchang... Read More

Jinsi ya Kujenga na kudumisha maelewano na uvumilivu katika uhusiano na mpenzi wako

Jinsi ya Kujenga na kudumisha maelewano na uvumilivu katika uhusiano na mpenzi wako

Kujenga na kudumisha maelewano na uvumilivu katika uhusiano na mpenzi wako ni muhimu sana kwa ustawi... Read More
Jinsi ya Kuwa Msaada wakati wa Shida na Msukumo wa mke wako

Jinsi ya Kuwa Msaada wakati wa Shida na Msukumo wa mke wako

Kuwa msaada wakati wa shida na msukumo kwa mke wako ni jambo muhimu katika kuimarisha uhusiano na ku... Read More
Kukabiliana na Mazoea ya Kutoelewana katika Mahusiano: Kusikiliza kwa Uelewa

Kukabiliana na Mazoea ya Kutoelewana katika Mahusiano: Kusikiliza kwa Uelewa

Mahusiano ni kitu ambacho kina changamoto zake, na moja ya changamoto hizo ni mazoea ya kutoelewa... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kiuchumi na kuwekeza

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kiuchumi na kuwekeza

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kiuchumi na kuwekeza ni jambo muhimu katika uhusiano... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Kuimarisha ushirikiano wa kijamii na familia ni muhimu sana katika kuendeleza mahusiano yenye fur... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kutoelewana katika Familia: Kusikiliza na Kuelewa Kwa Uaminifu

Kukabiliana na Mazoea ya Kutoelewana katika Familia: Kusikiliza na Kuelewa Kwa Uaminifu

Kukabiliana na Mazoea ya Kutoelewana katika Familia: Kusikiliza na Kuelewa Kwa Uaminifu

Fa... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Mshikamano katika Familia: Kuweka Nafasi ya Kujenga Urafiki

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Mshikamano katika Familia: Kuweka Nafasi ya Kujenga Urafiki

  1. Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Mshikamano katika Familia: Kuweka Nafasi ya Kujenga Urafiki... Read More
Kujenga Mawasiliano ya Amani na Furaha katika Familia Yako

Kujenga Mawasiliano ya Amani na Furaha katika Familia Yako

Leo hii, tutajadili umuhimu wa kujenga mawasiliano ya amani na furaha katika familia yako. Kwa ku... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Mara nyingi, wanaume wamekuwa wakipata wakati mgumu kuwa na uhusiano mzuri na msichana. Inawezeka... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About