Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Kujenga Ushirikiano wenye Ukarimu na Ujumuishaji katika Familia

Kujenga Ushirikiano wenye Ukarimu na Ujumuishaji katika Familia

Familia ni sehemu muhimu sana ya maisha yetu kama binadamu. Lakini ni muhimu kufahamu kwamba ili ... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo yenye Matokeo Matarajio na Wanafamilia

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo yenye Matokeo Matarajio na Wanafamilia

Mazungumzo ni sehemu muhimu sana ya uhusiano wa familia. Hata hivyo, kama si kwa ustadi, mazungum... Read More

Je, ni muhimu kwa washiriki wote kufikia kilele wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni muhimu kwa washiriki wote kufikia kilele wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni muhimu kwa washiriki wote kufikia kilele wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Wakati wa... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mipango ya Baadaye katika Familia: Kuweka Maono ya Pamoja

Jinsi ya Kuwa na Mipango ya Baadaye katika Familia: Kuweka Maono ya Pamoja

  1. Kuanzisha mawasiliano ya wazi: Ili kuweza kufikia malengo ya pamoja kama familia, ni mu... Read More

Jinsi ya Kugawana Majukumu ya Nyumbani na mke wako

Jinsi ya Kugawana Majukumu ya Nyumbani na mke wako

Kugawana majukumu ya nyumbani ni muhimu katika kujenga usawa na ushirikiano katika ndoa. Hapa kuna n... Read More
Jinsi ya Kusaidia na kushiriki katika malezi ya watoto na mpenzi wako

Jinsi ya Kusaidia na kushiriki katika malezi ya watoto na mpenzi wako

Kusaidia na kushiriki katika malezi ya watoto ni muhimu katika kujenga uhusiano mzuri na mpenzi wako... Read More
Wosia mzuri wa baba kwa mwanae

Wosia mzuri wa baba kwa mwanae

Mwanangu, mimi baba yako nimeishi miaka mingi kuliko wewe ndio maana unaniita baba. Ni kweli sija... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Mahusiano ni s... Read More

Je, kuna tofauti za kitamaduni katika mtazamo wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za kitamaduni katika mtazamo wa ngono/kufanya mapenzi?

Habari za leo wapenzi wa Kiswahili! Leo tutajadili suala la tofauti za kitamaduni katika mtazamo ... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano na Kusaidiana ili Familia Iwe na Amani na Furaha

Kuhamasisha Ushirikiano na Kusaidiana ili Familia Iwe na Amani na Furaha

Kuhamasisha Ushirikiano na Kusaidiana ili Familia Iwe na Amani na Furaha

Familia ni nguzo ... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijinsia wenye Kuridhisha katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijinsia wenye Kuridhisha katika Familia

  1. Kuhamasisha ushirikiano wa kijinsia wenye kuridhisha katika familia ni jambo muhimu lin... Read More

Kuendeleza na Kuimarisha Familia Yako: Mipango ya Baadaye

Kuendeleza na Kuimarisha Familia Yako: Mipango ya Baadaye

Kuendeleza na Kuimarisha Familia Yako: Mipango ya Baadaye

Familia ni kitovu cha maisha yet... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About