Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho ni muhimu katika kujenga uelewa na hesh... Read More
Jinsi ya Kusaidia Watoto kukabiliana na Hisia na Changamoto za Kihisia

Jinsi ya Kusaidia Watoto kukabiliana na Hisia na Changamoto za Kihisia

Mara nyingi watoto huwa na changamoto za kihisia kama vile huzuni, wasiwasi, na hata hasira. Kwa ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki wa kijamii

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki wa kijamii

Kujenga na kudumisha urafiki wa kijamii ni muhimu sana katika uhusiano. Hapa kuna njia kadhaa za kus... Read More
Ulinzi wa Kinga: Je, Matumizi ya Kinga ni Jambo la Lazima?

Ulinzi wa Kinga: Je, Matumizi ya Kinga ni Jambo la Lazima?

Karibu kwenye makala hii kuhusu ulinzi wa kinga na umuhimu wake. Kila siku tunajikuta tukiwa kati... Read More

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Kusisimua na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Kusisimua na Msichana Wako

Tarehe ya kusisimua inaweza kuwa ngumu kupanga, hasa ikiwa unataka kumpendeza mpenzi wako. Lakini... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Tarehe ya Kimapenzi na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Tarehe ya Kimapenzi na Msichana

Kama wewe ni miongoni mwa wanaume wanaotaka kuwa na tarehe ya kimapenzi na msichana, kuna vidokez... Read More

Jinsi ya Kudumisha Heshima na Utu katika Familia: Kuheshimu Tofauti na Upekee

Jinsi ya Kudumisha Heshima na Utu katika Familia: Kuheshimu Tofauti na Upekee

Familia ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunakua na kujifunza maadili y... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kujenga Malengo ya Fedha Pamoja

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kujenga Malengo ya Fedha Pamoja

Habari zenu wapenzi wasomaji, leo tutaangazia juu ya "Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na ... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Uaminifu katika Familia: Kuhamasisha Uaminifu na Urejesho

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Uaminifu katika Familia: Kuhamasisha Uaminifu na Urejesho

Katika maisha yetu ya kila siku, tunakabiliana na changamoto mbalimbali katika familia zetu. Moja... Read More

Jinsi ya kueleza hisia zako kwa mke wako

Jinsi ya kueleza hisia zako kwa mke wako

Kueleza hisia zako kwa mke wako ni muhimu katika kuimarisha uhusiano wenu na kujenga ufahamu wa kina... Read More
Njia za Kujenga Heshima na Usawa katika Kufanya Mapenzi: Kupigania Mahusiano ya Kijinsia yenye Afya

Njia za Kujenga Heshima na Usawa katika Kufanya Mapenzi: Kupigania Mahusiano ya Kijinsia yenye Afya

Mapenzi ni sehemu muhimu sana ya maisha yetu, lakini wakati mwingine yanaweza kuwa magumu kuyashu... Read More

Njia za Kupata Msichana Anayeshiriki Maslahi yako na Malengo

Njia za Kupata Msichana Anayeshiriki Maslahi yako na Malengo

Kupata msichana ambaye anashiriki malengo yako na ana maslahi sawa nawe ni muhimu sana kwa mafani... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About