Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Wosia mzuri wa baba kwa mwanae

Featured Image

Mwanangu, mimi baba yako nimeishi miaka mingi kuliko wewe ndio maana unaniita baba. Ni kweli sijasoma kama wewe ulivyosoma Ila mambo niliyokutana nayo tangu nimezaliwa ni elimu tosha ambayo wewe huna. Sasa nataka nikupe Elimu hiyo ili ukijumlisha na elimu yako ya darasani ujue namna nzuri ya kuishi katika dunia hii iliyojaa mishangazo mingi.

Maisha ni jumla ya mambo yote unayoyatenda kila siku. Namaanisha kila unalolifanya Leo linaathiri maisha yako ya kesho kwa hali chanya au hali hasi. Na kama ni hali hasi ni kwa ukubwa gani halikadharika kama ni hali chanya ni kwa kiwango gani. Mwanangu kila jambo unalolifanya Leo huamua ni mlango gani Unaweza ingia Kesho lakini pia mlango upi huwezi ingia Kesho. Ndio maana ni muhimu kuijua Kesho yako ukiwa Leo.

Mwanangu ili ufanikiwe ni lazima ujue kuishi na watu vizuri. Na mimi sikushauri kabisa kwamba uwe na marafiki wengi. Kuwa na marafiki wengi ni moja ya eneo unaweza jitengenezea mtego mbaya wa kukuangamiza kesho yako. Mwenye hekima mmoja aliwahi kusema ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe. Mwanangu kwa kusema hivyo simaanishi uwe na maadui,hapana. Ila marafiki zako watakusaidia mlango unaotaka kuingia Kesho uingie kwa urahisi au kwa ugumu au usiingie kabisa na wakati mwingine Unaweza kuingia na wakahusika kukutoa kwa aibu kubwa. Ndio maana ni muhimu Kuwa na marafiki ila Kuwa nao wachache chagua kwa makini mno. Sio lazima kila akufaaye kwa dhiki ndiye awe rafiki. Kuna watu wanakufaa kwa dhiki Leo ila Kesho wakutumikishe Kuwa makini sana.

Mwanangu, kuwa makini sana na mahusiano yako ya kimapenzi maana yanagusa hisia zako na mtu unayehusiana naye moja kwa moja. Hivyo basi kuwa makini maana mahusiano hayo yanaweza kukufanya Kesho ukamkosesha raha utakayekuwa naye kama sio huyo uliyenaye leo ndie ukajaaliwa Kuwa naye Kesho. Mwanangu, Unaweza kuniona mshamba sababu ulimwengu wenu unaonekana kama haujali sana haya mambo ila tafadhari zingatia utakapofika Kesho utaelewa sana hiki ninachokuambia.

Mwanangu, jichunge sana na mambo unayoyafanya Leo na uwe muungwana na kupenda haki. Tamaa isikupeleke ukafanya mambo mabaya ambayo yatakulazimisha kutunza siri moyoni mwako hata kama utafika ile Kesho yako. Jiepushe kabisa na mambo mabaya ya siri ya nafsi. Hakuna utumwa mbaya kama utumwa ndani ya nafsi yako mwenyewe maana kila ukikumbuka nafsi itakusuta na kukukosesha raha ya kweli. Hivyo kubali na kuridhika na ulivyo kama huwezi kujiongeza kwa njia halali na za haki. Ni heri uwe masikini mwenye uhuru ndani kuliko uwe tajiri na maarufu mwenye siri mbaya ndani ya Moyo wako. Mwanangu tafadhari uwe makini sana.

Mwanangu, siwezi sahau kukwambia kuhusu Mungu. Maisha ya uchaji wa Mungu yatakuepusha na mengi. Hapa naomba unielewe kwamba usijifanye unamcha Mungu bali mche Mungu. Sio kwasababu unashida ya kufanikiwa ndio umche Mungu, hapana! Bali umche Mungu sababu ni Mungu na yeye ndiye anaijua Kesho yako vizuri kuliko wewe mwenyewe. Ukimshirikisha mambo yako na ukawa mwaminifu kwake hakika hatakuacha kamwe.

Mwanangu, usiku umeenda nenda kalale sasa ila usije ukapenda na kutamani waovu kwa uovu wao na wakakushawishi ujiunge nao. Tafadhari usikubali.

#Kizazi Ganzi#

JIFUNZE KUJIFUNZA

Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki niย Soft copy [pdf]ย kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuwa Mfano wa Uvumilivu na Uwazi katika Familia: Kujenga Uhusiano Thabiti

Jinsi ya Kuwa Mfano wa Uvumilivu na Uwazi katika Familia: Kujenga Uhusiano Thabiti

Karibu katika makala hii ya jinsi ya kuwa mfano wa uvumilivu na uwazi katika familia, ili kujenga... Read More

Jinsi ya Kuwa na Muda Mzuri na Msichana Bila Kutumia Fedha Nyingi

Jinsi ya Kuwa na Muda Mzuri na Msichana Bila Kutumia Fedha Nyingi

Kutumia fedha nyingi kupata muda mzuri na msichana siyo lazima. Kuna njia nyingi za kuwa na muda ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na Kuunga Mkono katika Familia: Nguvu ya Ushirikiano

Jinsi ya Kusaidiana na Kuunga Mkono katika Familia: Nguvu ya Ushirikiano

Familia ni kitu muhimu sana katika maisha yetu. Inatupa nguvu, faraja, na upendo. Hata hivyo, kun... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na Kupumzika na Kujenga Utulivu na mke wako

Jinsi ya Kusaidiana na Kupumzika na Kujenga Utulivu na mke wako

Kusaidiana na kujenga utulivu na mke wako ni muhimu katika kuimarisha uhusiano wenu. Hapa kuna maele... Read More
Jinsi ya Kusaidiana katika kufanya maamuzi muhimu kuhusu elimu na malezi ya watoto wenu

Jinsi ya Kusaidiana katika kufanya maamuzi muhimu kuhusu elimu na malezi ya watoto wenu

Hakuna jambo jingine la muhimu katika maisha ya mwanadamu kama elimu na malezi kwa watoto wetu. K... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Ushirikiano katika Mahusiano: Kuhamasisha Ushirikiano wa Timu

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Ushirikiano katika Mahusiano: Kuhamasisha Ushirikiano wa Timu

Mahusiano muhimu kati ya watu yanategemea sana ushirikiano. Ni muhimu sana kuzingatia ushirikiano... Read More

Njia za Kuunganisha na Kuwa na Furaha katika Familia Yako

Njia za Kuunganisha na Kuwa na Furaha katika Familia Yako

Kuwa na furaha katika familia ni jambo muhimu sana kwa afya ya kiroho na kimwili. Kama mtaalamu w... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na wafanyakazi wenzake

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na wafanyakazi wenzake

Wakati mwingine, inaweza kuwa changamoto kupata njia ya kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga ... Read More

Jinsi ya Kuunganisha Kupitia Mchezo: Furaha na Uhusiano wa Familia

Jinsi ya Kuunganisha Kupitia Mchezo: Furaha na Uhusiano wa Familia

Karibu kwenye makala hii ambayo itakufundisha jinsi ya kuunganisha kwa furaha na uhusiano wa fami... Read More

Kujenga Mipaka na Kuheshimu Mipaka ya Kila Mtu ili Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Kujenga Mipaka na Kuheshimu Mipaka ya Kila Mtu ili Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Kujenga mipaka na kuheshimu mipaka ya kila mtu ni muhimu sana katika kuwa na amani na furaha kati... Read More

Je, ni njia gani zinaweza kuleta hisia za kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni njia gani zinaweza kuleta hisia za kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni njia gani zinaweza kuleta hisia za kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Swali hili lin... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za wanyama na utunzaji wa mazingira

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za wanyama na utunzaji wa mazingira

Jinsi ya Kuwasiliana na Mpenzi Wako Kuhusu Masuala ya Haki za Wanyama na Utunzaji wa MazingiraRead More

๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About