Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Featured Image

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi. Kidogokidogo alianza kupoteza urembo wake.
.
.
.

Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda, na mke alimpenda sana mumewe.
.
.
.

Siku moja mke alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume.
Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.
.
.
.

Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: โ€œSasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.โ€

Akajibu: โ€œMimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.โ€
.
.
.

FUNZO:

Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.

Meno huungโ€™ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa KUSAMEHEANA. Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa UMOJA.

1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza KUZUNGUMZA.

2. Ukiwa peke yako unaweza KUFURAHI, lakini ukiwa na mwenzako unaweza KUFURAHIA.

3. Ukiwa peke yako unaweza KUTABASAMU, lakini ukiwa na mwenzako mnaweza KUCHEKA.

Huo ndio UZURI wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana.

Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.

*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.

Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa umoja.
.
Tafakari
Mm na ww tunaweza kufanya haya!!!

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki niย Soft copy [pdf]ย kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Mbinu za kumfanya mwanamke akukubali

Mbinu za kumfanya mwanamke akukubali

Njia za kumfanya akukubali ni kama ifuatavyo

Uwe na muonekano mzuri

Wanawake wana... Read More

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Leo tutazungumzia njia za kujenga ushawishi na msichana katika uhusiano. Kujenga ushawishi kunama... Read More

Kukabiliana na Migogoro katika Uhusiano: Mbinu za Mazungumzo na Ushirikiano

Kukabiliana na Migogoro katika Uhusiano: Mbinu za Mazungumzo na Ushirikiano

Leo hii, tutazungumzia kuhusu kukabiliana na migogoro katika uhusiano. Hakuna uhusiano bila migog... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Mipango ya Pamoja katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Mipango ya Pamoja katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Mipango ya Pamoja katika Familia

Katika famil... Read More

Sifa Bora za Mwanamke: Jinsi ya Kumvutia Msichana Sahihi

Sifa Bora za Mwanamke: Jinsi ya Kumvutia Msichana Sahihi

Sifa Bora za Mwanamke: Jinsi ya Kumvutia Msichana Sahihi

Kila mwanaume anatamani kumpata m... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Fedha katika Familia Yako

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Fedha katika Familia Yako

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Fedha katika Familia Yako

Kila fam... Read More

Kuendeleza Upendo na Ushawishi katika Uhusiano wako

Kuendeleza Upendo na Ushawishi katika Uhusiano wako

Kuendeleza Upendo na Ushawishi katika Uhusiano wako

Kuendeleza upendo na ushawishi katika ... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Heshima na Uwazi katika Familia

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Heshima na Uwazi katika Familia

Kama unataka kuwa na familia yenye amani na furaha, mazungumzo ya heshima na uwazi ni muhimu sana... Read More

Mbinu 9 za kuwavutia na kuwateka wanawake kimapenzi

Mbinu 9 za kuwavutia na kuwateka wanawake kimapenzi

Kati ya wanawake na wanaume wote wawili wanahitaji kuvutiwa na wenza wao il... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano na Kushiriki Pamoja ili Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano na Kushiriki Pamoja ili Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Kuwa na amani na furaha katika familia ni jambo muhimu sana kwa afya ya kila mwanafamilia. Ni muh... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia historia na uzoefu wa mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia historia na uzoefu wa mpenzi wako

Kuelewa na kushughulikia historia na uzoefu wa mpenzi wako ni muhimu kwa kuimarisha uhusiano wenu na... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na mabadiliko katika uhusiano na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na mabadiliko katika uhusiano na mpenzi wako

Mabadiliko ni sehemu ya asili ya maisha na yanaweza kutokea katika uhusiano wako na mpenzi wako pia.... Read More
๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About