Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE 🔁
☰
AckyShine

Vyakula vya kukusaidia kupunguza uzito

Featured Image
Kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua uzito ni jambo tu la kula kalori chache na kufanya mazoezi zaidi. Hata hivyo, si mara zote zoezi hili linakuwa rahisi. Kama ni lengo lako kupunguza uzito, kuchagua chakula gani ule ni muhimu kama kuchagua kiasi gani cha chakula ule. Ukweli ni kwamba , baadhi ya vyakula vinauwezo wakusaidia kupunguza uzito kutokana na tabia zake za kuunguza mafuta mwilini.

Vifuatavyo ndivyo vyakula vinavyosaidia kupunguza uzito:

Mafuta ya Nazi

Mafuta ya nazi yanapanda chati kwa haraka kabisa na kufanya kuwa mojawapo ya vyakula bora kabisa kwa afya ya binadamu. Mojawapo ya vitu muhimu kabisa katika mafuta haya ni uwezo wake wa kupunguza uzito wa mwili. Mafuta ya nazi ni yana kemikali yenye mlolongo wa kati wa mafuta (“Medium Fatty Chain Acids”) ambayo humeng’enywa tofauti na yale yenye mlolongo mrefu wa mafuta (“Long Fatty Chain Acids”) Kemikali zenye mlolongo mrefu wa mafuta(“Long Fatty Chain Acids”) hupatikana kwa wingi katika vyakula vingi vya mafuta kaa vile nyama, chips n.k. Kemikali zenye mlolongo wa kati wa mafuta hutumiwa na mwili kwa ajili ya nishati badala ya kuhifadhiwa kama mafuta katika mwili. Hii ndio sababu mafuta ya nazi ni moja ya vyakula vyenye uwezo wa kuchoma mafuta mwilini na kusaidia kupungua uzito.

Siki ya Apple (Apple Cider Vinegar)

Siki ya Apple ina kiwango kikubwa cha kemikali za amino (amino acids) ,kemikali za kumeng’enya chakula na madini na vitamini. Utafiti unaonyesha kwamba kutumia Siki ya Apple kabla ya kula vyakula vya wanga inasaidia kupunguza kupanda kwa insulin hivyo kusaidia kutopata hamu ya kula mara kwa mara.

Ndimu na Limao

Utafiti unaonyesha kuwa kiasi cha vitamini C mwilini kinahusiana na uzito wa mwili. Watu wenye viwango vya kutosha wa vitamini C wana uwezo wa uwezo wa kuvunja asilimia 30 zaidi ya mafuta wakati wa mwili unapofanya shughuli za nguvu kama kazi za nyumbani,shambani na mazoezi kama kutembea, kuliko wale walio na kiwango cha chini cha vitamini C. Kama una dhamira ya kupungua uzito, basi fikiria kuanza siku yako kwa kunywa glasi moja ya maji yenye ndimu au limao au anza kutumia siki(vinegar) kwenye kachumbali au saladi unapokula chakula.

Balungi

Balungi yana kiasi kidogo cha kalori , kiwango cha juu cha tindikali za kumeng’enya chakula na inaweza kukufanya usijisikie njaa kwa muda mrefu. Watafiti wamegundua kwamba kula nusu ya balungi kabla ya mlo ni inachangia sana kupoteza uzito . Pia kula nusu tu ya balungi kabla ya mlo inaweza kusababisha kupungua kwa kiasi cha glucose-insulin katika muda wa masaa mawili tu. Kama wewe unahitaji kupungua uzito zingatia kula vyakula vinavyo kata mafuta na ongeza vyakula hivi vilivyotajwa katika mlo wako. Kwa mafanikio ya muda mrefu , kazania kula vyakula kamili (vyakula visivyo kobolewa au kusindikwa) na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia papai

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia papai

Dawa nyingine madhubuti ya chunusi ni papai. Tunda hili ni moja ya matunda yanayotumika kwa ajili... Read More

Dondoo kuhusu tezi dume

Dondoo kuhusu tezi dume

Tezi dume kila mwanaume anazaliwa nayo ambayo inasaidia kutoa maji maji ambayo yanaweza kusaidia ... Read More

Hizi ndizo faida za kiafya za kuota jua

Hizi ndizo faida za kiafya za kuota jua

Kuna mambo ambayo huwa tunayachukulia ya kawaida na wala hatuko tayari kufahamu umuhimu wake. Jua... Read More

Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kw... Read More
Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia mvuke

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia mvuke

Mvuke husaidia kusafisha ngozi. Ni rahisi sana kutumia mvuke kutibu chunusi.

Chemsha maji k... Read More

Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Kula lishe bora

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula... Read More

Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka

Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka

👉Kutibu shinikizo la chini la damu kwa kutumia maji chum... Read More

JE UNAFAHAMU NINI KUHUSU KUJAMBA?

JE UNAFAHAMU NINI KUHUSU KUJAMBA?

Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka?
Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi... Read More

Vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume

Vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume

Vifaa vya kieletroniki

Vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa ... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia baking soda

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia baking soda

Moja ya sababu za kutokea chunusi katika ngozi yako ni kuwepo kwa takataka au uchafu juu ya ngozi... Read More

Faida 8 za kula pilipili mbuzi

Faida 8 za kula pilipili mbuzi

Watu wengi tumekuwa hatufahamu utumiaji wa pipilipili, hasa pilipili mbuzi. Naomba leo tuangalie ... Read More

Madhara ya kunywa soda

Madhara ya kunywa soda

Tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dum... Read More

📖 Explore More Articles