Tatizo la maumivu wakati na baada ya kufanya mapenzi
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Wakati wa kufanya tendo la ndoa wapo baadhi ya watu hupatwa na maumivu wakati au baada ya kushiriki tendo, Maumivu haya yaweza kuwa;- Wakati tu uume unaingia,
Unapoingiza kitu chochote hata kidole, Wakati uume ukiwa ndani na Maumivu ya kupita (throbbing pain) yanayodumu masaa kadhaa baada ya tendo.
Sababu za maumivu
Sababu zaweza kuwa za kimwili (physical) au za kisaikolojia.
Sababu za kimwili baadhi ni kama;
Kutokua na ute wa kutosha kwa ajili ya kulainisha uke kutokana na kukosa maandalizi ya kutosha, kupungua kwa homoni baada ya ukomo wa hedhi, kujifungua au kunyonyesha, baadhi ya dawa za magonjwa ya akili, presha na uzazi wa mpango.
Ajali au upasuaji maeneo ya nyonga, ukeketaji na kuongezewa njia wakati wa kujifungua. Pia matibabu ya kutumia mionzi eneo la nyonga.
Tatizo la mishipa ya uke kusinyaa yenyewe (Vaginismus).
Tatizo la uumbaji linalopelekea mtu kuzaliwa wakati uke haujatengenezwa vizuri mfano โvaginal agenesis na imperforate hymen.โ
Magonjwa ya kizazi kama โendometriosis, PID,fibroids.โ
Sababu za kisaikolojia;
Msongo wa mawazo, wasiwasi, sonona, matatizo ya mahusiano, woga wa mimba, historia ya kuumizwa kimapenzi (sexual abuse) siku za nyuma.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Kuna mambo ambayo huwa tunayachukulia ya kawaida na wala hatuko tayari kufahamu umuhimu wake. Jua...
Read More
Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu w...
Read More
Dawa nyingine madhubuti ya chunusi ni papai. Tunda hili ni moja ya matunda yanayotumika kwa ajili...
Read More
Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na ...
Read More
Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wak...
Read More
Mchanganyiko wa mdalasini na asali ni dawa nzuri ya kutibu chunusi.
Changanya asali viji...
Read More
Mambo mhimu ya kuzingatia
1. Fanya mazoezi ya viungo kwa saa moja kila siku
2. Kunyw...
Read More
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kw...
Read More
Ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo ...
Read More
Watu wengi hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake. Hata hivyo mbali na kuwa na ladha n...
Read More
Kulingana na baadhi ya chunguzi zilizofanywa na wanasayansi asilimia 60 โ 70 ya wanaume hupotez...
Read More
JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*
*1.Usichelewe kwenda HAJA.* Kutunza...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!