Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Featured Image

Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)

Hii ni aina ya mizinga inayotumika sana na wengi. Gharama yake ni ndogo kiasi kulinganisha na mingine. Ni aina nzuri sana kwa mtu anaeanza ufugaji wa nyuki kwa kuwa ni wa gharama nafuu. Mfugaji wa nyuki anaweza kutengeneza mzinga Yya aina hii mwenyewe kama ana utaalamu wa useremala.
ย 
Mzinga wa Top bar
Faida ya Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar) โ€ข Ni rahisi kukagua asali iliyo tayari. โ€ข Ni rahisi kuvuna asali kuliko kuvuna toka kwenye mzinga wa kienyeji. โ€ข Ni rahisi kuwatunza nyuki wakati wa kiangazi na inapokuwa hakuna maua. Kwa mfano unaweza kuwapatia nyuki chakula ili kuongeza uzalishaji wa asali. โ€ข Ni rahisi kurina asali ukilinganisha na mizinga ya magogo inayotundikwa juu ya mti, kwa kuwa haihitaji vifaa maalumu. โ€ข Aina hii ya mizinga huwekwa kwa kuninginia jambo ambalo siyo rahisi kushambuliwa na wadudu/wanyama wanaokula asali kwa kuwa Inajaa haraka sana wakati ambao ni msimu wa asali kutengenezwa kwa wingi. Hasara ya Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar) โ€ข Kichane kwenye mzinga wa boksi hakina kishikizo hivyo huvunjika kwa urahisi sana kama hakitashikwa kwa uangalifu. โ€ข Masega huvunwa pamoja na asali, kwa hiyo nyuki wanalazimika kutengeneza tena masega mengine ambapo husababisha kupungua kwa uzalishaji wa asali.

Mzinga wa Langstroth

Mzinga wa Langstroth unaweza kukupatia asali zaidi kulinganishwa na mizinga mingine Hii ni aina nzuri na rahisa sana ya mzinga. Mizinga hii hufahamika kama mzinga wa fremu, kwa kuwa ina fremu ambazo vichane vya masega hujishikiza. Chumba kikubwa ambacho malkia hutagia mayai. Malkia anazuiliwa kuhama kwenda chumba kingine kwa kutumia waya. Kwenye chemba maalumu ya kutagia juu yake pana chemba ya kuhifadhia asali.
ย 
ย 
Mzinga wa Langstroth
Vichane vya masega vinatengezwa kwenye fremu na si kwenye nguzo kama ilivyo kwenye Top bar. Ili kuvuna asali, mfugaji akiwa na masega yaliyojaa asali, hutumia vifaa maalum kwa ajili ya urinaji na kuhifadhi asali bila kupata tabu. Mzinga wa Langstroth ni gharama kiasi kulinganisha na mizinga mingine.Unaweza kuipata kutoka katika taasisi zinazojiusisha na uuzaji wa mizinga, taasisi na karakana binafsi, au wakala wa Serikali.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Kirui Kipgeon (Guest) on August 24, 2026

Kenya

Kirui Kipgeon (Guest) on August 24, 2026

Hello dear ukoaje sasa

Related Posts

Siri ya kilimo cha nyanya kwa faida

Siri ya kilimo cha nyanya kwa faida

NYANYA HASA KWENYE OPEN SPACE CHANGAMOTO NI NYINGI, HASA WADUDU, KAMA SASA ... Read More

Matumizi ya mihogo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

Matumizi ya mihogo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

Muhogo Inazuia Minyoo na vidukari.

Hatua za Kutayarisha dawa

Mchanganuo wa Tsh 300,000/= kwa uzalishaji wa kuku wa kienyeji kwa faida

Mchanganuo wa Tsh 300,000/= kwa uzalishaji wa kuku wa kienyeji kwa faida

Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao... Read More

Mbinu za kulima parachichi ili kupata faida

Mbinu za kulima parachichi ili kupata faida

Kilimo cha Parachichi nacho kinalipa ukilima.

Kware au Read More

Faida ya kupanda maharagwe katikati ya kabichi

Faida ya kupanda maharagwe katikati ya kabichi

Maharagwe yanapandwa kwenye kabichi yanafanya kazi zifuatazo;

Kudhibiti wadudu (... Read More

Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana

Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana

"Cannibalism,"
Kudonoana kwa kuku ni tatizo linalo wa sumbua wengi, ni m... Read More

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waha... Read More

Ugonjwa wa tetanasi au pepopunda unaoathiri sana punda na binadamu

Ugonjwa wa tetanasi au pepopunda unaoathiri sana punda na binadamu

Huu ni ugonjwa hatari sana kwa maisha ya binadamu. Kinyesi cha punda kinabe... Read More

Jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji kitaalamu na kwa urahisi

Jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji kitaalamu na kwa urahisi

Mbolea ya mboji hutokana na mabaki ya majani na miti. Majani na miti yanapooza hugeuka na kutenge... Read More

Namna ya kulisha kuku ili wasipatwe na magonjwa

Namna ya kulisha kuku ili wasipatwe na magonjwa

Safisha vyombo vya kulishia na kunyweshea kila siku. Osha, sugua vizuri, kisha suuza kuondoa utando ... Read More
Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

1. Nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote kuzuia ueneaji na kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa ... Read More
๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About