Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote

Featured Image

Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoido…..leo nimetoka Likizo Moshi,

"Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa" hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!

Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!…kamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?…kwa Style ipi?

Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!…sasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,…hakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,….hapa sasa nikapata wazo!

"Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?''

"Mia mbili tu Kaka!"

''Ok"

Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,

"Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?" (Nilihamaki)

"Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?'''

Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!…Sasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!…My God kweli Body la "One Pack " haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!

"Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?"

Kimya…

"Dogo huu Mzani vipi?"

Kimya…

Dogo ana dharau huyu!…Sasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!….ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!…Dogo hakuwepo!….na Mabegi pia hayapo!…lap top haipo!….NIMEPIGWA!

Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!….sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!…yaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!…niitieni Ambulance!

πŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌ

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Nahida (Guest) on July 10, 2022

Hii ni kichekesho kali sana, ninashiriki na kila mtu! πŸ˜‚

Lucy Wangui (Guest) on June 25, 2022

πŸ˜‚πŸ‘πŸ˜…πŸ€£

Rashid (Guest) on May 16, 2022

Hii ni dhahabu ya vichekesho! πŸ˜„

Charles Mchome (Guest) on May 7, 2022

Asante Ackyshine

Agnes Lowassa (Guest) on May 2, 2022

Brilliant! Muda wake ulikuwa kamili! ⏰

Josephine Nekesa (Guest) on April 24, 2022

Hii ni joke ya maana sana! πŸ˜‚πŸ‘Œ

Peter Otieno (Guest) on March 29, 2022

Hizi jokes ni za ukweli! πŸ˜†πŸ‘

Richard Mulwa (Guest) on March 16, 2022

Kila siku napenda jokes zenu! πŸ˜†πŸ˜‚

Margaret Anyango (Guest) on March 16, 2022

Hii imenichekesha sana! πŸ˜„πŸ˜‚

Elijah Mutua (Guest) on March 10, 2022

Kweli mna kipaji cha ucheshi! πŸ‘πŸ€£

Samson Mahiga (Guest) on January 5, 2022

🀣πŸ”₯😊

Lydia Mzindakaya (Guest) on December 31, 2021

Hizi jokes zinabamba sana! πŸ˜†πŸ˜‚

Lydia Mahiga (Guest) on December 22, 2021

Hii ni joke ya kipekee sana! πŸ˜‚πŸ‘

George Mallya (Guest) on December 15, 2021

πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜†πŸ˜…

Joy Wacera (Guest) on November 23, 2021

Ucheshi wenu unanifurahisha kila siku! πŸ˜ŠπŸ˜‚

Dorothy Mwakalindile (Guest) on October 17, 2021

Hii ni joke ya ukweli kabisa! πŸ˜‚πŸ€£

Nancy Kawawa (Guest) on July 24, 2021

Ucheshi wenu ni wa hali ya juu! πŸ‘πŸ€£

Paul Kamau (Guest) on July 23, 2021

Hii ni kali sana! πŸ˜‚πŸ€£

Joyce Aoko (Guest) on July 21, 2021

πŸ˜ŠπŸ˜‚πŸ˜…πŸ‘

Samuel Were (Guest) on July 20, 2021

Hii kichekesho imenifurahisha sanaβ€”imebamba! 🀣

Lydia Wanyama (Guest) on June 28, 2021

Bado nacheka, hiyo ilikuwa nzuri sana! 🀣

Faith Kariuki (Guest) on June 27, 2021

πŸ€£πŸ€£πŸ‘πŸ˜†

Agnes Njeri (Guest) on June 10, 2021

Hii imenibamba sana! πŸ˜…πŸ€£

Salum (Guest) on May 28, 2021

πŸ˜‚ Sijacheka hivi kwa muda mrefu sana!

Edwin Ndambuki (Guest) on May 27, 2021

πŸ˜„ Hii ni ubunifu wa hali ya juu!

Linda Karimi (Guest) on April 5, 2021

Hii imenifurahisha sana! 🀣😊

Simon Kiprono (Guest) on March 26, 2021

Hii ni aina ya kichekesho usichosahau! πŸ˜‚

Grace Njuguna (Guest) on March 17, 2021

πŸ€£πŸ˜„πŸ˜Š

John Kamande (Guest) on March 14, 2021

Hii ndio nilihitaji leo! Asante! 😜

Lydia Wanyama (Guest) on March 11, 2021

πŸ˜… Bado ninacheka!

Esther Nyambura (Guest) on February 17, 2021

Hii ni joke ya kipekee! πŸ€£πŸ‘Œ

Elizabeth Mrope (Guest) on February 13, 2021

πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜…

Anna Mahiga (Guest) on February 10, 2021

Hii imenipa kicheko cha siku! πŸ˜‚πŸ˜†

Joseph Kiwanga (Guest) on January 20, 2021

Huyu alikuwa na point! πŸ˜‚πŸ‘Œ

Arifa (Guest) on January 17, 2021

Hii kichekesho imebadilisha kabisa hali yangu! πŸ˜ƒ

Jane Muthui (Guest) on January 10, 2021

Napenda jokes zenu! πŸ˜ŠπŸ˜…

Michael Mboya (Guest) on December 4, 2020

Nimecheka hadi nimesahau shida zangu! πŸ€£πŸ˜†

Lucy Kimotho (Guest) on December 3, 2020

Umetisha! πŸ‘ŒπŸ˜‚

Daudi (Guest) on November 26, 2020

πŸ˜„ Umenishika vizuri!

Patrick Kidata (Guest) on November 19, 2020

πŸ˜†πŸ˜‚πŸ˜Š

Mary Sokoine (Guest) on November 8, 2020

πŸ˜…πŸ˜ŠπŸ˜‚πŸ‘

Mwanais (Guest) on November 5, 2020

πŸ˜„ Kichekesho gani!

Sarafina (Guest) on October 30, 2020

πŸ˜… Nilihitaji kicheko hiki, asante!

Michael Mboya (Guest) on October 29, 2020

Huu ucheshi hauna kifani! 🀣πŸ”₯

Moses Kipkemboi (Guest) on October 25, 2020

Hii imenifurahisha sana! πŸ˜ŠπŸ˜…

Mwakisu (Guest) on October 13, 2020

🀣 Sikutarajia hiyo!

John Lissu (Guest) on September 12, 2020

Hii imenikuna sana! πŸ˜†πŸ˜…

John Mwangi (Guest) on July 9, 2020

Nimecheka hadi nimesahau shida! πŸ€£πŸ˜†

Peter Mugendi (Guest) on June 29, 2020

Nimeipenda hii joke! πŸ˜„πŸ˜‚

Alice Mwikali (Guest) on May 25, 2020

Lazima niihifadhi hii, ni kichekesho kali sana! πŸ˜†

John Mushi (Guest) on May 9, 2020

Kweli mnajua kuchekesha watu! πŸ€£πŸ˜‚

Michael Onyango (Guest) on May 2, 2020

πŸ˜† Ninaihifadhi kwa baadaye!

Anthony Kariuki (Guest) on April 28, 2020

πŸ˜„ Umeshinda mtandao leo!

Alice Mwikali (Guest) on April 20, 2020

Nimefurahia sana hii! πŸ˜…πŸ˜Š

Nancy Komba (Guest) on March 25, 2020

😁 Kicheko bora ya siku!

David Sokoine (Guest) on March 22, 2020

Nimecheka hadi machozi yanatoka! 🀣😭

Diana Mallya (Guest) on February 5, 2020

😁 Hii ni dhahabu!

Esther Nyambura (Guest) on February 2, 2020

Kweli mna ucheshi! πŸ˜‚πŸ€£

Sharifa (Guest) on January 4, 2020

πŸ˜… Nilihitaji kicheko hicho!

Rose Kiwanga (Guest) on December 19, 2019

Hii imenipa kicheko cha siku! πŸ˜‚πŸ€£

Related Posts

Hizi sifa zimezidi sasa

Hizi sifa zimezidi sasa

MADEM KWA SIFA..

kuumwa aumwe yeye lakn kujifanya anajali sana bas utam... Read More

Utoto raha..! Angalia hawa watoto wanachokifanya sasa

Utoto raha..! Angalia hawa watoto wanachokifanya sasa

Leo nimepulizia Air Fresh yenye Harufu ya Pilau nyumbani kwangu sasa watoto wa Jirani wamehamia ... Read More

MAMBO KUMI YA KUFURAHISHA NA HUWEZI KUYAFANYA

MAMBO KUMI YA KUFURAHISHA NA HUWEZI KUYAFANYA

1. Huwezi kuosha Macho kwa Sabuni;
2. Huwezi kuhesabu Nywele zako;

3. Huwezi kupumua k... Read More

Kilichotokea Baada ya mlevi na mchungaji kukutana

Kilichotokea Baada ya mlevi na mchungaji kukutana

MCHUNGAJI; "Unakunywa bia!?
MLEVI; "Ndio.
MCHUNGAJI; "Kwa siku unakun... Read More

Angalia huyu jamaa alivyomuweza huyu binti wa chuo

Angalia huyu jamaa alivyomuweza huyu binti wa chuo

😁😁😁😁 .. TABU KUDATE NA MADEMU WA CHUO
Demu ;Β Baby Safari Hii N... Read More

Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!

Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!

Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. ... Read More

Hii sasa ni kali

Hii sasa ni kali

Siku izi kujuana kumezidi hata ukienda msibani kama hauna connection hauli msosi

πŸ˜‚πŸ˜... Read More

Soma hii, Nani haelewi kati ya hawa?

Soma hii, Nani haelewi kati ya hawa?

Dogo: Bro naomba nitumie hela.

Bibi na Babu walisafiri wakielekea kwa mtoto wao ambae hawajamuona zamani.<... Read More

Cheki huyu jamaa anachomfanyia huyu mrembo kanisani

Cheki huyu jamaa anachomfanyia huyu mrembo kanisani

Jamaa kaenda kanisani akakaa karibu na mrembo. Wakati mahubiri yakiendlea jamaa akaanza kuingiza voc... Read More
Wazo la jioni hii

Wazo la jioni hii

πŸ“’WAZO LA JIONI HII πŸ“’

KAMA MWAKA JANA ULIPIGA HATUA NA HUJAFIKIA MALENGO MWAKA HUU... Read More

Chezea kufulia!

Chezea kufulia!

Huu Mwezi jinsi nilivyofulia yaani hata nikikuta mende wamesimama wawili najua wananisem... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About