Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.


UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Kutafuta Furaha: Mambo Mazuri Katika Kufanya Mapenzi

Kutafuta Furaha: Mambo Mazuri Katika Kufanya Mapenzi

Kutafuta Furaha: Mambo Mazuri Katika Kufanya Mapenzi

Kila mtu anatamani furaha katika mape... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maamuzi muhimu ya kifamilia

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maamuzi muhimu ya kifamilia

Kuwajibika na kufanya maamuzi muhimu ya kifamilia ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kudumu. Hapa kuna ... Read More
Jinsi ya Kusimamia Majukumu ya Kazi na Familia: Kujenga Usawa na Ufanisi

Jinsi ya Kusimamia Majukumu ya Kazi na Familia: Kujenga Usawa na Ufanisi

Jinsi ya Kusimamia Majukumu ya Kazi na Familia: Kujenga Usawa na Ufanisi

Hivi karibuni, ma... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mvuto wa Kipekee kwa Msichana

Jinsi ya Kuwa na Mvuto wa Kipekee kwa Msichana

Kila mtu anataka kuwa na mvuto wa kipekee kwa msichana. Lakini je, unajua jinsi ya kuwa na mvuto ... Read More

Jinsi ya kushirikiana na mke wako katika Kulea Watoto

Jinsi ya kushirikiana na mke wako katika Kulea Watoto

Kushirikiana na mke wako katika kulea watoto ni muhimu katika kujenga familia yenye nguvu na yenye u... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiimani na mafundisho ya kidini na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiimani na mafundisho ya kidini na mpenzi wako

Kama unapenda mtu wa imani tofauti na wewe, hapa kuna maoni kadhaa ambayo yanaweza kukusaidia kue... Read More

Njia za Kupitia Matatizo ya Fedha katika Uhusiano wako

Njia za Kupitia Matatizo ya Fedha katika Uhusiano wako

Habari Rafiki yangu, leo tutazungumzia njia za kupitia matatizo ya fedha katika uhusiano wako. Kw... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kushughulikia maumivu na majeraha ya kihisia

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kushughulikia maumivu na majeraha ya kihisia

Kushughulikia maumivu na majeraha ya kihisia ni muhimu katika kujenga na kudumisha uhusiano wenye af... Read More
Ushauri kwa mwanamke anayetafuta Mwanaume ili upate Mume sahihi

Ushauri kwa mwanamke anayetafuta Mwanaume ili upate Mume sahihi

Siku zote mwanamke hawezi pata mwanaume aliye sahihi,,,.

1. Ukimpata handsome,,kichwa yake ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha uhusiano na jamaa

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha uhusiano na jamaa

Kujenga na kudumisha uhusiano na jamaa ni muhimu katika maisha ya kifamilia. Hapa kuna miongozo ya j... Read More
Kujenga Mazingira ya Upendo na Kujali katika Familia Yako

Kujenga Mazingira ya Upendo na Kujali katika Familia Yako

Familia ni moja ya mazingira muhimu kuliko yote katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunakulia, t... Read More

Jinsi ya Kujenga Uaminifu katika Familia: Kuheshimu na Kutimiza Ahadi

Jinsi ya Kujenga Uaminifu katika Familia: Kuheshimu na Kutimiza Ahadi

Leo, tutajadili jinsi ya kujenga uaminifu katika familia kwa njia ya kuheshimu na kutimiza ahadi.... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About