Log in to access your menu with tools for managing ๐ tasks, ๐ฅ clients, ๐ฐ finances, ๐ learning, ๐ personal growth, and ๐ spirituality, all in one place!.
eBooks: Biashara - Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti - Topic 2 - AckySHINE
Kuwa na kawaida ya kujiwekea Akiba ni njia na Siri ya kuwa tajiri
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:30 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wengi wanajiuliza, โSiri ya utajiri ni nini?โ Je ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwaya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa naziada na faida.
Updated at: 2024-05-23 16:07:15 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
KILA mtu duniani ana ndoto ingawa haijalishi ni ndoto gani uliyonayo. Ndoto uliyonayo ina thamani kubwa kuliko fedha wala kitu chochote kile. Ndoto uliyonayo ina nguvu kubwa ya kubadilisha maisha yako na kukufikisha sehemu ambayo ulitaka ufike ama zaidi ya pale ulipotarajia kufika.
Ndoto yako inaweza kukupeleka sehemu mbalimbali duniani ukazunguka kufanya mambo yako si kwa sababu una fedha sana, bali ni kwa sababu una ndoto. Ni vyema utambue nguvu ya ndoto uliyonayo ni kubwa kuliko fedha.
Umasikini isiwe sababu wala utajiri isiwe sababu ya kuwa mchafu au kutokuwa na usafi
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:35 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Umasikini sio sababu ya kuwa mchafu wala utajiri Sio kuwa na kila kitu hata kama hukihitaji. Hebu angalia hapo nyumbani kwako!
Vitu msivyovihitaji Leo wala kesho mmeweka vya nini? Umenunua makochi mapya Yale ya zamani mmegawana vyumbani mnaishia kurundika minguo hapo na kufuga mipanya.
Godoro umenunua jipya la zamani umeviringisha juu ya kabati. Kabatini kwako kuna nguo ulivaa ukiwa secondary mpaka Leo unazo eti ukumbusho au utazivaa ukipungua.
Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:06 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jiwekee utaratibu utakaokupa uzoefu wa kuamua vizuri juu ya fedha unazopata. Watu tumekuwa tukitumia fedha tunazopata bila kufikiria jinsi ya kugawa ktk matumiz badala yake baada ya kutumia ndio una/ninaanza kujuta Kwa nin nime/umetumia tofauti na mahitaji uliyonayo. Kiasi cha fedha ulichonacho chaweza kukufanya uwe maskini au tajir kutokana na maamuz unayofanya juu ya hiyo fedha.
Updated at: 2024-05-23 16:07:13 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
kadri temperature inavyo ongezeka chura nae huwa ana increase temperature ya mwili wake..
pindi inapokaribia kufika boiling point yaani nyuzi 100 chura atashindwa kuongeza temperature ktk mwili wake na hapo ndipo atataka kutoka ktk maji hayo ya moto na yanayo endelea kuchemka.. kutokana na kutumia nguvu nyingi sana ktk kuongeza temperature ktk mwili wake,pindi anapotaka kuruka atashindwa na atakufa humo ndani ya chombo cha maji yanayochemka..
Updated at: 2024-05-23 16:07:25 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utakuwa mwisho wa matatizo yangu na kuwa huru kufanya kila kitu ninacho kitaka. ๐๐๐๐๐ Sasaa baada ya kuipata iyo kazi nimekuja kupata ukweli kwamba kumbe kazi ya kuajiriwa siyo Mwarobaini wa Yale niliyo Nayo kumbe ndiyo safari inaanza na siyo mwisho kama nilivyo dhani.
Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:12 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA! ๐ฅMama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika.
Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:10 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Siku moja nilichukua taxi aina ya UBER nikiwa naelekea uwanja wa Ndege Mwl. Nyerere Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara. Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu.
Wewe ni mshindi: Mambo yakuzingatia ili uweze kushinda chochote katika maisha
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:23 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mshindi ni mtu aliyeshinda, Hivyo wewe ni mshindi kwa kuwa umeshinda, kuwa hai leo ni ushindi, kuwa na Mungu mpaka sasa huo ni Ushindi, kuweza kujifunza semina na kufuatilia mafundisho kama haya wewe ni mshindi. Ebu jiulize ni watu wangapi ulikuwa unawafahamu leo hawapo duniani? Wewe umeshinda Mungu kakuweka duniani ili uendelee kushinda.
Updated at: 2024-05-23 16:07:32 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
UJASIRIAMALI
Ni uthubutu au ujaribu wa ufanyaji wa shughuli yoyote halali na kupitia shughuli hiyo mtu watu huweza kupata kipato.
ย
MJASIRIAMALI
Ni mtu mwenye yeyote mwenye uthubutu au kujaribu kufanya shughuli yoyote halali,ambapo kupitia shughuli hiyo anaweza kupata kipato ambacho kitamfanya apige hatua ya kimaendeleo ya kiuchumi.Shughuli za kijasiliamali zinaweza kuwa za biashara ya uzalishaji mali au bidhaa.
Ushauri wangu kwa leo: Zingatia hili, hamasika, badilika
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tupo kwenye dunia ambayo tulikuta watu na tutawaacha watu. Vyote tulivyovikuta vilianzishwa na binadamu wengine wenye mawazo mema na wenye mawazo mabaya pia. Vitu vingi tunavyovifanya tunaendeleza tulivyovikuta ni mara chache kukuta kitu kipya ambacho hakitegemei mazingira na asili ya tulivyovikuta.
Updated at: 2024-05-23 16:07:17 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo
Siri 39 za kuwa Milionea, Jinsi ya kupata pesa na kuwa tajiri
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:16 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
1. Tafuta fursa kila kona. 2. Tumia kipaji chako. 3. Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk. 4. Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.
Updated at: 2024-05-23 16:07:12 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.
Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?
Kwa nini kuna matajiri na maskini na wote tunapewa masaa 24??? Tucheki mgawanyo Wa masaa 24 ulivyoโฆ.katika masaa 24 unayopewa kwa siku masaa 8 ni ya kazi,masaa 8 ni ya kulala na masaa 8 ni ya kufanya mambo yako mengine.
FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:29 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha yao yatachukua miaka mingi sana kabla hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia fursa moja tu.
Updated at: 2024-05-23 16:07:34 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ikiwa leo ni tarehe **1/12ย huwezi amini kuwa hakuna tarehe 1 nyingine tutakayoiona ya mwaka huu hivyo sichelei kusema kuwa mwaka umeisha .Lakini mwaka unaishaje??? pengine hili ndilo swali gumu na la muhimu la kujiuliza .Je, Mwaka unaisha ukiwa umefanya nini cha kujipongeza??? .Je mwaka unakaribia kuisha maarifa yako yakiwa yameongozeka kwa kiasi gani???.Haya ni maswali muhimu sana unavyooanza kufikiria juu ya sherehe za mwisho wa mwaka.
Updated at: 2024-05-23 16:07:20 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
1.๐ฅUmejipa jukumu la kuwa "mpelelezi" wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.
2.๐ฅUmebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.
3.๐ฅ Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!
Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:00 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jifunze kanuni za fedha kama ilivyoainishwa hapo chini. Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kutumia Hii kanuni inatumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani
USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:03 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.
Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.
Updated at: 2024-05-23 16:07:22 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna watu wengi sana huwa wanani-challenge ninaposema kwamba ni muhimu sana mtu kuishi katika kusudi la maisha yake. Na moja kati ya hoja zao ni kwamba haya maisha ya sasa mtu akisema aanze kutafuta kusudi la maisha yake atakufa maskini. Hivyo wanaonelea ni bora kufanya chochote kitakachotokea mbele yake ilimradi mwisho wa siku anapata pesa. Yaani anachagua kuwa mtumwa wa Pesa
Updated at: 2024-05-23 16:07:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Siku hizi kuna tangazo moja la kampuni ya simu za mikononi, Tigo, likimuonesha mama akiwa _busy_ na pembeni yupo mwanae mdogo apo akijisemesha na akatamka maneno ambapo mama akaona ni kama ameanza kuongea. Kwa furaha anampigia simu mumewe akimtaka amsikilize mwanae akiongea. Hapo mama anamtaka mwanae aseme "mama" na baba naye anavutia kwake akimtaka aseme "baba". Kwa maajabu kabisa mtoto anawapotezea wote na kutamka "ni Tigo peesa". Wazazi wakashikwa na butwaa lakini huku wakitabasamu.
Updated at: 2024-05-23 16:07:22 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tafuta fursa kila kona. Tumia kipaji chako. Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.
Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyoteย - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.
Updated at: 2024-05-23 16:07:07 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wengi tunapenda sana Pesa lakini hatuko tayari kuzifanyia Pesa kazi nikiwa na maana kutumia njia sahihi kuzipata na tunapozipata hatuna Akili ya kuweza kuwa nazo muda mrefu zisiondoke. Kama tujuavyo katika maisha yetu haya Pesa ndio kila kitu,tunahitaji Pesa ili tuweze kufanya mambo mengi mazuri na makubwa.Kitu kinachotukwamisha hatujui tufanye nini ili tuweze kuzipata hizi Pesa na tunapozipata tunakosea tena cha kuzifanyia ili zisipotee tena au zisiishe.
AMINI UNA AKILI YENYE UWEZO MKUBWA WA KUBUNI WAZO LA KUWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKIWA KIMAISHA
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:05 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Huwa nikikaa na kufikiri ni namna gani binadamu aliweza kubuni ndege, meli kubwa hasa za mizigo, gari na vitu vinginevyo na badae kuja kuwa msaada mkubwa katika dunia yetu ya siku leo hata kurahisisha maisha katika eneo fulani lililokuwa na ugumu kwetu, basi nauona uwezo wa Mungu aliouweka ndani ya binadamu huyu ingawa yeye binafsi kama binadamu wakati mwingine hatulitambui hilo na kama tunalitambua basi ni wachache na wakati mwingine hatujakaa vizuri kuitumia hii fursa ya uwezo huo tuliopewa. Hii inaonyesha ni jinsi gani binadamu alivyo na uwezo mkubwa wa kufanya ubunifu kwa kupitia akili aliyonayo na kuleta mageuzi na mshangao mkubwa katika ulimwengu tunaoishi.